Tuesday, June 7, 2011

Simba yatangaza viingilio mechi kati yao na DC Motema Pembe hapo jumapili.


 Send to a friend
Tuesday, 07 June 2011 20:07
Clara Alphonce
UONGOZI wa Simba umesema kuwa tayari umemtafutia kocha Moses Basena mikanda miwili ya video ya mechi za DC Motema Pembe huku wakitanga viingilio vya mchezo wa Jumapili.Simba watakaribisha Motema Pembe jijini Dar es Salaam katika harakati za kusaka kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekwisha kamilika na tayari wamekwisha watumia tiketi za kuja Dar es Salaam waamuzi wa mchezo huo kutoka Nigeria na kamisaa ambaye anatoka Sudan watatua hapa nchini Ijumaa.

Kaburu alivitaja viingilio kuwa ni 20,000 kwa  VIP A, 10,000 kwa VIP B-C, viti vya rangi ya machungwa 8,000 huku viti vya bluu na kijani ni 5,000.

Alisema mpaka sasa bado hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa wapinzani wao kuwa watatua nchini lini kwa ajili ya mchezo huo japo tayari kocha wao amekwishaona mikanda ya michezo yao miwili na kuifanyia kazi.

Alisema wachezaji wao wana hali na mchezo huo baada ya kupoteza mchezo wao na Wydad na pia wanataka kumuonyesha kocha wao Basena kuwa wanauwezo mkubwa na yale yaliotokea Misri ni makosa ambayo hawata yarudia tena.

Pia, alisema timu hiyo wanayocheza nayo sio ngumu sana kwani walikwishaiona wakicheza na KMKM ya Zanzibar na kuona ni timu ambayo haitishi sana hivyo ni kazi kwao wachezaji kuwaopa wapenzi wao raha kwa kuwafunga magoli mengi hapa nyumbani.

Alisema nia ya kuweka viingilio vya chini ni kuwataka watanzania wote kuja kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao ambayo ni timu pekee inayowakilisha nchi katika michuano ya kimataifa katika klabu.

Alisema timu imerejea Dar es Salaam jana wakitokea mkoani Tanga ambako walikuwa wameweka kambi ya siku kadhaa na kuendelea na maandalizi ya mchezo huo.

Alisema wachezaji ambao walikuwa kwenye timu zao za taifa tayari wameanza kuwasili kwa Emmanuel Okwi kuwasili toka juzi huku Jerry Santo alitua jana akitokea Angola alipokuwa akichezea Harambee Stars.

No comments:

Post a Comment