Send to a friend |
Send to a friend |
Tuesday, 07 June 2011 20:03 |
0digg YAOUNDE, CameroonSERIKALI ya Cameroon imesema watu wanne wamefariki kutokana na vurugu iliyotokea baina ya mashabiki na polisi baada ta timu ya taifa ya Cameroon kulazimishwa suluhu Senegal kwenye mchezo wa kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani. Afisa wa polisi aliimbia Associated Press Jumatatu kuwa vurugu za Jumamosi kati ya mashabiki wenye hasira na vikosi vya jeshi pia yalisababisha watu wengi kuumia. Hakusema ni watu wangapi walioumia au waliouwawa ni wanajeshi au raia. Viongozi hao wameomba radhi kwa kutokea tukio hilo.Nahodha wa Cameroon, Samuel Eto’o alikosa penalti dakika ya mwisho iliyogonga mwamba na kuwaacha mabingwa hao mara nne wa Afrika kwenye nafasi ya tatu katika Kundi E. Polisi walitumia maji kuwatawanya mashabiki hao waliovamia basi lililochukua wachezaji na kuvunja vioo wakati likitoka kwenye Uwanja wa Ahmadou Ahidjo jijini Yaounde, baada ya kukaa ndani kwa zaidi ya saa moja huku mashabiki hao wakimshutumu Eto'o kuwa ndiyo chanzo cha matatizo ya timu hiyo. Mshambuliaji hiyo wa Inter Milan aliomba radhi kwa mashabiki hao kupitia redio ya taifa. “Kwanza nawashukuru kwa kutuunga mkono muda wote wa mchezo,” alisema. “Nimekosa penalti. Nathahili lawama zote za kupoteza mchezo huu. Naomba sana msahama kwa hili. Hii ndiyo penalti pekee niliyokosa katika msimu huu.” Shuti la Eto’o liligonga mwamba kwenye muda wa majeruhi na kuifanya Cameroon kukosa ushindi muhimu kwenye mchezo huo.Cameroon kwa sasa ina pointi tano nyuma ya vinara Senegal iliyokaribia kufuzu moja kwa moja ikiwa na mechi mbili mkono. Mshambuliaji wa Monaco, Benjamin Moukandjo naye alikosa nafasi kadhaa za wazi za kufunga kwa Cameroon iliyotawala sehemu kubwa ya kipindi cha pili kusaka bao la ushindi. |
No comments:
Post a Comment