Thursday, September 1, 2011

Wapinzani waaza kuikimbia Igunga

venance.chadema@yahoo.com


Thursday, 01 September 2011 09:34


WAKATI vuguvugu la siasa jimboni Igunga mkoani Tabora likiendelea kushika kasi, wapinzani wameanza kuukimbia uchaguzi huo, kufuatia mgombea wa TLP, Dk Moses Edward kujitoa katika kinyan’anyiro hicho.

Akizungumuza na waandishi wa habari jana katika ofisi za chama hicho jimboni Igunga, Dk Edward alisema uamuzi huo wa kuachia ngazi mapema ni kutoa nafasi kwa chama chake kujipanga vizuri kwa ajili ya chaguzi zijazo.

Aliahidi kwamba  Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, TLP itamsimamisha mgombea kwenye jimbo hilo na wanaamini atashinda bia wasiwasi wowote.
 
Kutokana na hatua hiyo, aliwataka wanachama na wapenzi wa TLP kumuunga mkono mgombea ambaye ataonyesha uwezo mkubwa wa kuwaletea maendeleo kulingana na sera watakazotoa kwenye kampeni hizo.

Dk Edward ambaye pia ni mwenyekiti wa TLP wilaya ya Igunga alieleza kuwa sababu za uamuzi wa kujitoa mapema kabla ya kampeni kuanza ni pamoja na maandalizi ya chama hicho kuwa hafifu katika uchaguzi huo mdogo huku vyama vingine vikiwa vimejizatiti vya kutosha.

Alifafanua kuwa chanzo kikuu cha kujitoa ni kukosa fedha na kwamba makao makuu ya TLP wameshindwa kumpa nguvu.

"Nimefikia uamuzi huu hasa kwa makao makuu ya chama changu kutotoa msaada wowote,’’ alilalamika mgombea huyo.

Mpaka sasa katika jimbo la Igunga hali ya kisiasa inazidi kuchukua sura mpya hasa mji huo kuwa na wanasiasa mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali nchini kwa ajiliya kuviongezea nguvu vyama vyao.

Wagombea sita mpaka sasa wamekwisha chukua fomu za kuwania nafasi ya ubunge iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wake, Rostam Aziz wa CCM ambaye alijiuzulu.

Kwenye uchaguzi huo Chadema imemsimamisha Joseph Mwandu, CUF Leopard Mahona, SAU John Maguma, DP  Said Makeni, UMD Lazalo Ndegaya na  CCM
Dk Peter Kafumu.

Dk Kafumu kuchukua fomu  
CCM imekuwa kwenye maandalizi makubwa ya kuhakikisha kwamba mgombea wake, Dk Kafumu anapewa mapokezi makubwa atakapoenda kuchukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kesho.

Katibu wa CCM wilaya ya Igunga, Neema Adam alisema mapokezi makubwa yanamsubiri wakati atakapowasili hapa akitokea Dar es Salaam ambako alienda kushuhudia Kamati Kuu ya chama hicho ikitamtangaza kuwa mgombea.

Alisema anatarajia kuwasili kesho na siku hiyo hiyo ataenda kuchukua fumu.

“Tunategemea kufanya mapokezi hayo kuanzia saa tatu au saa nne kwa kuwa sasa hivi hayupo hapa, na tumeandaa pikipiki, mikokoteni baiskeli kwa kuwa siku hiyohiyo atacukua fomu.

Mtei na Rostam
Wakati huo huo, Mwandishi Mosses Mashalla anaripoti kutoka Arusha kuwa, Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei amesema kuwa kitendo cha CCM kuamua kumtumia mbunge aliyejiuzulu kwenye jimbo hilo, Rostam kwenye kampeni za uchaguzi huo mdogo, kitawagharimu.

Lakini akasema maadamu CCM imeamua kumpeleka Rostam ambaye ni mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi kifanye mpango wa kuwapeleka wote wenye shutuma za namna hiyo.

“Kitendo cha kumpeleka Rostam kinaonyesha hawa watu wamechoka hawawezi kupambana na ufisadi.

Alisema kuwa wao kama Chadema watatumia mkakati huo wa CCM kama sehemu ya kujiibulia kura kwa kuweka hadharani kashfa zake.

Hatahivyo, alisisitiza ya kuwa watawaeleza wakazi wa Igunga  namna ya kuchambua mchele na pumba.

Mashidano ya bendera
Baadhi ya vyama vinavyowania Ubunge wa jimbo la Igunga katika uchaguzi mdogo unatorarajiwa kufanyika Oktoba 2 mwaka huu, vimekuwa katika mapambano ya kuweka bendera za vyama vyao.

Bendera za vyama hivyo zimekuwa zikionekana kutundikwa kwenye nguzo za umeme na maeneo mbalimbali ya Igunga mjini.

No comments:

Post a Comment