9 Disemba, 2011 - Saa 12:00 GMT
Klabu ya Manchester United imethibitisha kua beki wake Nemanja Vidic hatoshiriki tena michuano ya msimu mzima.
Beki huyo aliondolewa uwanjani kwa machela baada ya kujeruhi goti lake wakati wa mechi kati ya Manchester United na Basel katika Ligi ya mabingwa.
Meneja wa Man.utd Sir Alex Ferguson amesema inasikitisha na ni habari mbaya kwamba tutamkosa Vidic kwa kipindi kizima cha msimu wa Ligi.
Ferguson alimtarajia kua huenda nahodha wake akakaa nje kwa mda mfupi na sio msimu mzima.
Aliongzea kusema kua ataonana na mtaalamu wa viungo siku ya jumatatu kubaini lini
afanyiwe upasuaji. Hilo haliwezi kufikiwa hadi watulize uvimbe.Uwezekano wa kuchukua mahali pake ni kati ya Evans, Phil Jones au Chris Smalling.
Ferguson anakabiliwa na kigezo cha kupoteza hadi wachezaji tisa jumamosi hii klabu yake itakapochuana na Wolves, mechi ambayo ilitarajiwa kua chachu ya ushindi baada ya matokeo mabovu ya miezi michache iliyopita.
Miongoni mwa wachezaji wasioweza kumsaidia Ferguson ni Michael Owen, Anderson, Tom Cleverley, Fabio, Rafael na Javier Hernandez pamoja na mshambuliaji wa upande wa kushoto Ashley Young alionekana kuzidi kutonesha jeraha la kidole chake katika mechi dhidi ya Basel ambapo ilibidi aondolewe mapeema kipindi cha pili.
Mshambuliaji Dimitar Berbatov, ambae amekua akiuguza gotio pia anatazamiwa kushiriki mechi dhidi ya Wolves.
No comments:
Post a Comment