Send to a friend |
Send to a friend |
Thursday, 08 December 2011 20:43 |
0digg MIAMBA ya Ligi Kuu ya England, Manchester United na Manchester City wametupwa nje kwenye Ligi ya Mabingwa huku Lyon ikifuzu kwa 16 bora kwa kishindo baada ya kufunga mabao saba. Mabingwa wa Ulaya mwaka 1968, 1999 na 2008, United, walitupwa nje baada ya kukubalia kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Basel, ushindi ulioipa nafasi timu hiyo ya Uswisi kuungana na Benfica kufuzu kutoka kwa Kundi C. City iliwafunga vinara wa Kundi A, Bayern Munich 2-0 , lakini wameshindwa kufuzu kwa 16 bora baada ya Napoli kuchukua nafasi hiyo kwa kuichapa Villarreal 2-0 nchini Hispania. Hii ni mara ya tatu katika miaka 17 ya Sir Alex Fergusuon kuishudia United ikishindwa kuvuka hatua ya makundi. Pamoja na kuhitaji pointi moja tu, mabingwa hao mara tatu waliduwazwa kwa kufungwa goli kila kipindi kutoka kwa Marco Streller na Alexander Frei yalitosha kukipa kipigo cha kwanza ugenini kwa kikosi cha Ferguson kwenye hatua hiyi baada ya miaka mitano kupita. Phil Jones alifunga bao dakika za majeruhi, lakini Basel waliweza kuhimili presha za United na kufanikiwa kukata tiketi yao kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo msimu wa 2002-03. Kwa United, iliyocheza nusu fainali tatu kati ya nne zilizopita, sasa wanakaribisha kwenye mashindano ya Europa Ligi. "Ni wazi tumeuzunika, na hakuna njia nyingine ya kufikiria nje ya hivyo," alisema Ferguson. "Ndio mpira. Unatakiwa ujifunze kupoteza pia, na kwa timu hii watatumia kama changamoto kwao." Kocha wa Basel, Heiko Vogel, ambaye alichukua mikoba ya Thorsten Fink mwezi Oktoba, alikuwa mwenye furaha isiyokifani. "Ni jambo la pekee, ndio, kwa sababu si kila siku utaweza kuifunga Manchester United," alisema. Pigo kubwa liliendelea kwenye jiji la Manchester, baada ya City nayo kutupa nje ya mashindano pamoja na David Silva na Yaya Toure kufunga 2-0 dhidi ya Bayern Munich iliyotumia kikosi cha pili baada ya wachezaji wake wengi kusumbuliwa na mafua. Vinara hao wa Ligi Kuu ya England, City waliingia kwenye mchezo huo wakijua kuifunga Bayern ambayo imeshafuzu kwenye Kundi A, isingetosha hadi pale Napoli itaposhindwa kuifunga Villarreal. Silva alifunga bao la kwanza kabla ya mapumziko kwenye Uwanja wa Eastlands na Toure alifunga la pili mwanzoni mwa kipindi cha pili. Lakini ushindi wa Napoli wa mabao 2-0 nchini Hispania ili maanisha timu ya Roberto Mancini sasa iweke nguvu zake katika kusaka ubingwa wa England na Europa Ligi. "Kwa kawaida ukiwa na pointi10 timu zote zinafuzu, kwa asilimia 99," alisema Mancini. "Hili ni kundi la ajabu, ilikuwa kundi gumu." Ushindi wa Napoli umewavusha kwa 16 bora kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21 wakati huo Diego Maradona akiwa bado mchezaji. Lyon ilifanya usiku wa aina yake baada ya kuisambaratisha Dinamo Zagreb 7-1 nchini Croatia huku wenyeji hao wakimaliza wachezaji 10 baada ya dakika ya 28 mchezaji wao Jerko Leko kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Lyon iliingia kwenye mchezo huo wa mwisho wa Kundi D ikiwa nyuma kwa pointi tatu kwa Ajax na ilitaji kushindi ili kupata tofauti ya mabao saba ili iweze kufuzu. Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa, Bafetimbi Gomis alithibisha ubora wake kwa kufunga mabao manne, pamoja na mabao matatu ya haraka zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa, Lyon imemaliza ya pili kutoka katika kundi hilo. Real Madrid, ambayo tayari imeshafuzu inayojiandaa na mechi ya kesho 'El Clasico' dhidi ya Barcelona, ilichapa Ajax 3-0 jijini Amsterdam na kuwa timu ya tano katika historia kufuzu bila ya kupoteza mchezo wowote. CSKA Moscow ilifuzu shukrani kwa bao la dakika tatu za mwisho kutoka kwa Vasili Berezutsky lililoipa ushindi timu hiyo ya Russia 2-1 dhidi ya Inter Milan kutoka Kundi B. Mshambuliaji wa Ivory Coast, Seydou Doumbia alifunga bao la kwanza kwa wageni kabla ya Esteban Cambiasso kusawazisha, lakini Berezutsky alifunga bao la ushindi kwa CSKA. Huku Trabzonspor wakiwalazimisha suluhu Lille. |
No comments:
Post a Comment