Showing posts with label Moses Mashalla. Show all posts
Showing posts with label Moses Mashalla. Show all posts

Tuesday, October 18, 2011

UVCCM waandamana Arusha.

venance.chadema@yahoo.com

 
Monday, 17 October 2011 21:34

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Arusha, James Ole Millya (katikati) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya Monduli, Julius Kalanga (kushoto) walipoungana na vijana wa jumuiya hiyo katika maandamano kutoka Makao Makuu ya Polisi mkoani humo kuelekea ofisi ya UVCCM mkoa, jana. Picha na Filbert Rweyemamu

KUNDI la wafuasi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha, jana lilizingira uzio wa Makao Makuu ya Polisi mkoani hapa ambako mwenyekiti wa umoja huo, James Milya alikwenda kujisalimisha.Wakati Milya akihojiwa, wafuasi hao wa CCM walibaki nje wakiimba nyimbo mbalimbali za kumsifu kiongozi wao huyo.

Wafuasi hao walifika hapo wakimsindikiza Milya kwa maandamano maalumu hali iliyowalazimisha polisi kuwazuia kuingia kwenye lango kuu. Walibaki huku kuendelea kuimba.

Milya aliwasili katika Ofisi Polisi Mkoa wa Arusha saa 6:30 mchana akiwa ndani ya gari aina ya Lexus. Mbali ya kusindikizwa na wafuasi wake hao, pia alikuwapo wakili wake, Moses Mahuna.

Baada ya kushuka kwenye gari hilo akiwa na wakili wake na baadhi ya viongozi wa UVCCM, aliekea moja kwa moja katika ofisi ya Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Akili Mpwapwa ambako alikaa huko kwa takriban dakika 15 kabla ya kutoka nje na kupokewa kwa shangwe na wapambe wake.

Baada ya Milya kutoka, maandamano makubwa ya

Friday, September 16, 2011

venance.chadema@yahoo.com
Uteuzi wakuu wa mikoa wawagawa wananchi
Thursday, 15 September 2011 20:52

Rais Jakaya Mrisho Kikwete

UTEUZI wa wakuu wapya wa mikoa uliotangazwa jana na Ikulu, umewagawa watu wa kada mbalimbali wakiwamo wasomi na wanasiasa.Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili wameukubali na wengine waliuponda.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana,  walioponda uteuzi huo walisema hauna jipya kwa sababu hata hao walioondoka hawakuweza kutatua kero za wananchi.

Mwasisi wa Chadema, Edwin Mtei, alisema haamini kama wateule hao wapya watakuwa na jipya na kwamba, uongozi wao hauwezi kuwa wa tija ikiwa Serikali haitabomoa mfumo wa utawala wake ambao alidai kuwa ni wa kifisadi.

“Huu uteuzi hauna jipya, wote ni wale wale tu kwani hata walioondoka hawakuweza kutatua kero za wananchi hawa walioingia nao wametoka katika mfumo uleule wa kifisadi,” alisema Mtei.

Mtei alieleza wasiwasi wake kuhusu utaratibu wa watu kupewa nyadhifa mbili akisema