| Sunday, 05 June 2011 20:58 |
| Happy Lazaro, Arusha WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Mount Meru, kimeomba serikali kuhakikisha inasimamia kikamilifu fedha za wanafunzi kupitia bodi ya mikopo. Wakizungumza kwenye hafla ya kuchagua uongozi mpya wa serikali ya wanafunzi wa chuoni hapo, walisema fedha hizo zimekuwa hazina usimamizi mzuri na kuleta usumbufu kwao. Rais anayemaliza muda yake, Ezekiel Meliary, alisema wanafunzi wengi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto lukuki, zinazotokana na bodi ya mikopo kutegemea fedha kutoka serikalini. Meliary alisema asilimia 98 ya wanafunzi wanaosoma shahada ya elimu na elimu ya biashara, wanategemea zaidi mikopo kutoka serikalini , hivyo bodi ya mikopo imekuwa tatizo kubwa. Alisema hali hiyo inasababisha kuwapo kwa migogoro wakati mwingine migomo isiyoisha kwenye vyuo |
Mahakama ya Uingereza
Mahakama kuu ya Kenya imekataa ombi la mbunge mashuhuri nchini humo Chris Okemo na aliyekuwa mkurugenzi Mkuu wa shirika la umeme la kitaifa Samwel Gichuru la kiuzuia serikali kuwakamata na kuwapeleka Uingereza kujibu mashtaka ya ufisadi na uhalifu wa kiuchumi.
Jaji Nicholus Ombiji ameshangaa kwanini wawili hao wanababaika kwa kufika mahakamani wakati serikali ya Kenya yenyewe bado haijawasilisha kesi ya kuomba wakamatwe na kufikishwa katika mahakama ya visiwa vya Jersey nchini Uingereza.
Mahakama imemwambia Okemo ambaye wakati mmoja alikuwa waziri wa nishati na pia waziri wa fedha wa

