| Send to a friend |
| Tuesday, 07 June 2011 20:07 |
Clara Alphonce UONGOZI wa Simba umesema kuwa tayari umemtafutia kocha Moses Basena mikanda miwili ya video ya mechi za DC Motema Pembe huku wakitanga viingilio vya mchezo wa Jumapili.Simba watakaribisha Motema Pembe jijini Dar es Salaam katika harakati za kusaka kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho. Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekwisha kamilika na tayari wamekwisha watumia tiketi za kuja Dar es Salaam waamuzi wa mchezo huo kutoka Nigeria na kamisaa ambaye anatoka Sudan watatua hapa nchini Ijumaa. Kaburu alivitaja viingilio kuwa ni 20,000 kwa VIP A, 10,000 kwa VIP B-C, viti vya rangi ya machungwa 8,000 huku viti vya bluu na kijani ni 5,000. Alisema mpaka sasa bado hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa wapinzani wao kuwa watatua nchini lini kwa |

