Tuesday, June 14, 2011

Mahakama yaamuru Askofu Mokiwa, Hoyay wakamatwe.


 Send to a friend
Monday, 13 June 2011 22:27
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa
Mussa Juma, Arusha
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha imeagiza kukamatwa mara moja na kufikishwa mahakamani, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa na Askofu mpya wa Kanisa hilo aliyewekwa wakfu juzi, Stanley Hotay.Askofu Mokiwa, alimweka wakfu Hotay Jumapili, siku mbili tangu Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutoa maagizo ya kusitishwa kwa shughuli hiyo.

Kitendo hicho cha Askofu Mokiwa kuendelea na mchakato wa kumweka wakfu Askofu Hotay pamoja na amri ya Mahakama kutaka shughuli hiyo isitishwe, kimeelezwa kuwa ni dharau kwa mahakama.

Sherehe za kuwekwa wakfu Askofu huyo zilifanyika juzi Makao Makuu ya Dayosisi ya Mount Kilimanjaro na zilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Isdore Shirima, Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Claudio Bitegeko na maofisa kadhaa kutoka vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Uamuzi wa kukamatwa kwa maaskofu hao, ulitolewa jana na Jaji Kakusulo Sambo baada ya wakili wa mashtaka, Meinrad D’souza kuwasilisha maombi maalumu ya kutaka Mahakama Kuu itoe adhabu kwa Dk Mokiwa na Hotay kwa kukaidi amri ya Mahakama.

Akitoa uamuzi ambao ulichukua takriban saa moja, Jaji Sambo alisema haihitaji elimu ya chuo

TUTAMFUKUZA ZITO, SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA


 Send to a friend
Monday, 13 June 2011 22:33

Zitto Kabwe
Waandishi wetu
VITA ya kufutwa posho za wabunge na watumishi wengine wa umma, imechukua sura mpya, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kusema kwamba Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe anaweza kufukuzwa ubunge kwa kutosaini karatasi za mahudhurio.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge baada ya kuahirisha mkutano wa asubuhi, Makinda alisema Zitto anaweza kukumbwa na adhabu hiyo iwapo hatasaini karatasi za mahudhurio ambazo ndizo zinazothibitsha uwepo wa mbunge katika mikutano na vikao vyake.

"Kwa mujibu wa kanuni zetu, asipohudhuria mara tatu anakabiliwa na adhabu tena ya kufukuzwa bunge, hizo ndivyo kanuni zinavyosema." Hata hivyo, Zitto amepuuza kauli hiyo ya Spika akisema kwamba kama ni kwa ajili ya kukataa posho, yuko tayari kufukuzwa bungeni.

"Nitafanya hivyo tuone. Kanuni inasema mikutano mitatu mfululizo na siyo vikao vitatu mfululizo. Nitatumia uzoefu wangu wa siasa za wanafunzi kukwepa mtego wake. Lakini kama anadhani ni sawa kunifukuza ubunge kwa kukataa posho, nipo tayari," alisema Zitto.

Kauli ya Makinda inafuatia msimamo wa Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), kukataa

Friday, June 10, 2011

Chadema yaichana Bajeti ya Serikali.


 Send to a friend
Thursday, 09 June 2011 23:37
Neville Meena, Dodoma
KAMBI ya Upinzani Bungeni imedai kwamba kuna upotoshaji mkubwa katika Bajeti ya Serikali iliyowasilishwa bungeni juzi na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, huku ikidai kwamba bajeti hiyo ni ya kulipa posho na madeni.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Kambi hiyo mjini Dodoma na kusainiwa na Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe inabainisha kuwa upembuzi uliofanywa umebaini kuwapo kwa upotoshaji mkubwa wa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa kwalengo la kuwajengea matumaini wananchi.
"Kambi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya Serikali kutenga zaidi ya robo ya bajeti kulipa madeni na kulipana posho (asilimia 27), asilimia 14 kulipa madeni na asilimia 13 kulipa posho mbalimbali," ilisema taarifa hiyo.
Miongoni mwa maeneo ambayo yanadaiwa kuwa na upotoshaji ni kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la umeme, ongezeko la jumla la Bajeti ya Serikali ikilinganishwa na ile ya mwaka 2010/11, posho mbalimbali, faini kwa madereva wazembe na ulipaji wa madeni ya Serikali.

Hakuna mradi mpya wa umeme
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tamko la Serikali kwamba imetenga kiasi cha Sh537 bilioni kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme, si kweli kwani kwa jumla Wizara ya Nishati na Madini, imetengewa Sh402.071 bilioni na kwamba hakuna mradi mpya wa umeme hata mmoja utakaoanzishwa.
"Fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya matumizi ya kawaida Sh76,953,934,000  na  kwa upande wa bajeti ya maendeleo zimetengwa Sh325,448,137,000. Sh325 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa 160 MW, 100 Dar es Salaam na 60 Mwanza,"inaeleza sehemu ya

CCM Arusha wamkataa rasmi Chatanda


 Send to a friend
Thursday, 09 June 2011 23:18
Moses Mashalla, Arusha na Patricia Kimelemeta, Dar
WENYEVITI wa CCM kutoka wilaya za Mkoa wa Arusha, wamekutana kujadili mgogoro wa chama mkoani humo na kutoa mapendekezo manne juu ya namna ya kumaliza mgogoro huo, ikiwamo kumwondoa Katibu wa CCM wa mkoa huo, Mary Chatanda.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa, kikao hicho kilifanyika Juni Mosi mwaka huu katika Jengo la CCM, Mkoa wa Arusha na kuhudhuriwa na wenyeviti wa chama kutoka wilaya za Arusha, Arumeru, Longido, Karatu, Monduli na Ngorongoro.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, wenyeviti hao walibaini kuwa Chatanda ni chanzo cha mgogoro huo, hivyo ni bora akahamishwa au kuondolewa kabisa katika nafasi hiyo ndani ya CCM.
Mapendekezo mengine yaliyofikiwa katika kikao hicho na wenyeviti hao ni Chatanda kuitwa na kuonywa ili aache kutoa matamko kinyume na taratibu za chama na kutaka itafutwe njia ya haraka kurejesha amani ndani ya UVCCM mkoani humo.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na wenyeviti hao kwenda kwa Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama, ambayo Mwananchi ina nakala yake, hali ya kisiasa ndani ya CCM mkoani Arusha ni tete.Barua hiyo ilidai kuwa, Chatanda ni chanzo cha mgogoro mkoani humo kwa kuwa anaendesha shughuli zake kwa ubabe, dharau, majivuno na

‘Wapinzani shirikini katika maendeleo ya taifa’


 Send to a friend
Thursday, 09 June 2011 20:32
Ally Mkoreha,
 Dodoma
VYAMA vya upinzani nchini, vimeshauriwa kujenga utamaduni wa kushiriki katika mambo ya msingi yanayohusu maendeleo ya taifa, ukiwamo Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano ili kuinua uchumi na kuwaondoa wananchi katika umaskini unaowakabili.

Ushauri huo ulitolewa jana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dk Philipo Mpango, alipokuwa akizungumza katika semina maalumu kwa wabunge, kuhusu mpango huo unaoanza katika mwaka 2011 hadi mwaka 2016, semina hiyo ilifanyika mjini Dodoma.
"Tunaviomba vyama vya upinzani, vishiriki katika utekelezaji wa mpango huu wenye manufaa makubwa kwa nchi yetu. Ni mpango ulioandaliwa kitaalamu na utasaidia katika kuinua uchumi wa nchi, tuwe kitu kimoja katika jambo hili. Vijana wetu wapewe nafasi kwa sababu ni wabunifu na wana ujuzi, wakisaidiwa, tatizo la ajira kwao litapungua," alisema Dk Mpango.

Rai hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ambaye alisema mpango huo ni wa taifa na wala siyo wa chama chochote cha siasa na kwamba hata CCM haipaswi kuunadi. Alisema kwa kuzingatia hilo, kila mwananchi ana wajibu wa kuchangia katika utekelezaji wa mpango huo ili ulete mafanikio yanayotarajiwa.

Akizungumzia mpango huo na kuuhusisha na hali ya sasa ya

Zitto ajitoa kupokea posho za Bunge, Naibu katibu wa bunge alitolea ufafanuzi, adai aliomba fedha yake ya posho ipelekwe kwenye akaunti ya maendeleo mkoa wa KIGOMA.Asema bunge haliwezi kufanya hivyo kwa madai sheria haruhusu.


 
Thursday, 09 June 2011 23:25

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
Venance Mrema
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuiomba isimamishe kumlipa posho zake zinazotokana na vikao vya Bunge kuanzia juzi.Zitto ametoa ombi hilo kwa barua rasmi aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah Juni 7 mwaka huu.
Katika barua hiyo, ambayo gazeti hili limefanikiwa kuiona, Zitto alisema anaamini kuwa watumishi wa Serikali na wabunge, hawastahili kulipwa posho wanapohudhuria vikao rasmi vya uwajibikaji wao wa kawaida.
Zitto alisema kuwa posho hiyo haistahili kulipwa kwake, wabunge wengine wala watumishi wa umma kwa kuwa kuhudhuria vikao ni sehemu ya kazi zao.
"Kwa mujibu wa Sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly Act of 2008) na kwa mujibu wa Masharti ya Kazi za Mbunge niliyokabidhiwa, ninastahili kupata posho za vikao, (sitting allowances) kila ninapohudhuria vikao vya Bunge na Kamati zake,"alisema Zitto na kuongeza:
"Ni imani yangu kuwa posho ya kikao haistahili kulipwa kwa mbunge na mtumishi mwingine yeyote wa Serikali kwani kuhudhuria kikao ni sehemu ya kazi yangu,".
Kupitia barua hiyo, Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha, alieleza kwamba amekuwa akipendekeza posho za vikao hivyo ifutwe, jambo ambalo pia limo katika mapendekezo ya chama chake (Chadema) katika Bajeti ya 2011/2012.
"Nimekuwa nikipendekeza kuwa posho hii ifutwe. Chama changu cha Chadema pia kimependekeza jambo hili katika mapendekezo yake ya Bajeti 2011/2012," alisema Zitto na kuendelea:
"Mpaka hapo mfumo wa kulipana posho za vikao utakapofutwa, ninaelekeza kwamba stahili zangu zote za posho zielekezwe katika Taasisi ya Kigoma Development Initiative (KDI).., utaratibu huu uanze kuanzia tarehe 8/6/2011."

Katibu wa Bunge agoma kuizungumzia
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alipoulizwa jana kama amepokea barua hiyo ya Zitto, alisema kuwa, yeye kama mtendaji wa mhimili huo wa Dola, anapokea barua nyingi, hivyo si rahisi kukumbuka kama barua hiyo imefika ofisini kwake.
Lakini akasema, hata kama barua hiyo itakuwa imemfikia ofisini, kanuni na taratibu haziruhusu Bunge kutangaza habari za mtu binafsi.Alisema ofisi yake hairuhusiwi kuandika masuala binafsi ya wabunge yanayofikishwa ofisini na

Tevez akashifu Manchester


Nahodha wa Manchester city Carlos Tevez amesema kuwa mmiliki wa klabu hiyo, Sheikh Mansour, amemruhusu kuondoka akitaka.
TevezMmiliki wa Man.city
Sheikh Mansour
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliwasilisha ombi la kuhama klabu hiyo katikati ya msimu uliopita kinyume na habari za kukanusha taarifa hizo.
Tevez alisema kuwa angependa kuihama Uingereza na

Muafaka kuhusu serikali ya mpito Somalia


Wafuasi wa Waziri mkuu mjini Mogadishu
Waziri Mkuu Mohammed anatakiwa kujiuzulu chini ya siku 30
Viongozi wa Somalia wamekubaliana kusitisha uhasama wa kisiasa kati yao baada ya mzozo uliodumu miezi kadhaa.
Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed na Spika wa Bunge Sheikh Sharif Aden wamekubaliana kuhairisha uchaguzi hadi mwezi Agosti mwaka ujao.
Utata huo wa viongozi umesababisha kuzorota kwa uhusiano kati ya serikali ya mpito na jumuiya ya

Marekani yataka Gaddafi ang'olewe haraka


Marekani imeyaomba mataifa ya Magharibi na ya Kiarabu kuongeza juhudi katika azma ya kumng'oa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.
Waziri wa mashauriano ya nchi za kigeni Bi Hillary Clinton amesema huu ndio wakati wa kumtimua Gaddafi.
Bi Clinton akihutubia mkutano wa Abu Dhabi
"Huu ni wakati wetu,mazingira yanaturuhusu.Gaddafi amefika kikomo'', Bi Clinton alisema katika mkutano wa viongozi wanaokutana mjini Abu Dhabi.

Bi Clinton pia aliwaambia wajumbe kuwa lazima juhudi zaidi zifanywe za kumbana Gaddafi na utawala wake kisiasa, kidiplomasia na

Tuesday, June 7, 2011

Eto'o aua mashabiki wanne


 Send to a friend
Tuesday, 07 June 2011 20:03
YAOUNDE, Cameroon
SERIKALI ya Cameroon imesema watu wanne wamefariki kutokana na vurugu iliyotokea baina ya mashabiki na polisi baada ta timu ya taifa ya Cameroon kulazimishwa suluhu Senegal kwenye mchezo wa kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani.

Afisa wa polisi aliimbia Associated Press Jumatatu kuwa vurugu za Jumamosi kati ya mashabiki wenye hasira na vikosi vya jeshi pia yalisababisha watu wengi kuumia.

Hakusema ni watu wangapi walioumia au waliouwawa ni wanajeshi au raia. Viongozi hao wameomba radhi kwa kutokea tukio hilo.Nahodha wa Cameroon, Samuel Eto’o alikosa penalti dakika ya

Simba yatangaza viingilio mechi kati yao na DC Motema Pembe hapo jumapili.


 Send to a friend
Tuesday, 07 June 2011 20:07
Clara Alphonce
UONGOZI wa Simba umesema kuwa tayari umemtafutia kocha Moses Basena mikanda miwili ya video ya mechi za DC Motema Pembe huku wakitanga viingilio vya mchezo wa Jumapili.Simba watakaribisha Motema Pembe jijini Dar es Salaam katika harakati za kusaka kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekwisha kamilika na tayari wamekwisha watumia tiketi za kuja Dar es Salaam waamuzi wa mchezo huo kutoka Nigeria na kamisaa ambaye anatoka Sudan watatua hapa nchini Ijumaa.

Kaburu alivitaja viingilio kuwa ni 20,000 kwa  VIP A, 10,000 kwa VIP B-C, viti vya rangi ya machungwa 8,000 huku viti vya bluu na kijani ni 5,000.

Alisema mpaka sasa bado hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa wapinzani wao kuwa watatua nchini lini kwa

Mkuu wa Majeshi ashangaa kulipwa pensheni ya Sh50,000


 Send to a friend
Tuesday, 07 June 2011 20:57
Filbert Rweyemamu, Arusha
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya ameitaka serikali kuangalia upya maslahi ya wanajeshi wastaafu akisema bado wanayo nafasi ya kulitumikia taifa kwani bado ni askari wa akiba kwa mujibu wa viapo vyao.

Akihutubia katika uzinduzi wa Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania (Muwawata), Mkoa wa Arusha, alisema yeye pamoja na kulitumikia jeshi kwa muda mrefu, ameweza kujenga kibanda cha kuishi yeye na familia yake huku akilipwa pensheni ya Sh50,000 kwa mwezi lakini akiwaona baadhi ya watumishi wa umma wakiwa na majengo ya kifahari katika miji mbalimbali nchini.

“Kuna watumishi wana majengo ya makubwa ambayo hayaendani na mapato yao, nasema haya kwa

Mbunge CUF, wenzake waachiwa kwa dhamana


 Send to a friend
Tuesday, 07 June 2011 20:54
Mustapha Kapalata,Tabora
HATIMAYE Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Magdalena Sakaya na wenzake 11 wameachiwa kwa dhamana.
Mbunge huyo na wenzake waliachiwa jana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Urambo, Oscar Bulugu, baada ya kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa na mahakama hiyo, ingawa walipunguziwa masharti waliyopewa awali.

Masharti magumu yalikuwa ni kwa washtakiwa wanaotoka nje ya Wilaya ya Urambo, wakati wanaotoka ndani ya wilaya hiyo walitakiwa kuwa na barua ya mtendaji wa kata na walitimiza masharti ya kuwa na barua hizo.

Washtakiwa wote walishindwa kutimiza masharti waliyopewa na mahakama Jumatatu na kulazimika kurudishwa mahabusu, lakini upande wa utetezi uliomba masharti hayo kwa wanaotoka nje ya

Mashambulizi ya Boko Haramu



Takriban watu watano wameuawa baada ya vituo vya polisi kushambuliwa katika mji wa Maiduguri ulioko kaskazini mwa Nigeria taarifa za hospitali zimesema.
Mandhari ya Maiduguri
Maiduguri
Mandhari ya Maiduguri
Mwandishi wa BBC Bilkisu Babangida aliyeko katika mji huo anasema kulikuwa na milipuko mitatu na milio ya risasi ilisikika katika kil kinachoaminika kuwa ni shambulio la kikundi cha Boko Haram.
Wafuasi wa kundi hilo Boko Haramu wameua maofisa wengi wa polisi pamoja na wanasiasa katika

Rais Saleh wa Yemen 'aliumia' sana


Saleh
Rais wa Yemen Ali Abdallah Saleh anayedaiwa kujeruhiwa vibaya
Rais wa Yemen, Ali Abdullah Saleh, alijeruhiwa zaidi katika shambulio la makombora katika boma lake juma lililopita kuliko ilivyodhaniwa, maafisa wa Serikali wameambia vyombo vya Habari vya Marekani.
Maafisa wa Serikali waliambia shirika la Habari la AP kuwa Bwana Saleh alichomeka asilimia 40 ya mwili wake na anavuja damu katika fuvu lake kutokana na shambulio hilo la Ijumaa.
Rais anaendelea kupata matibabu nchini Saudi Arabia baada ya kushambuliwa katika Ikulu yake katika Mji Mkuu wa Yemen, Sanaa.
Afisa wa cheo cha juu Serikalini aliambia BBC kuwa hawatasema lolote kuhusiana na afya ya Rais Saleh.
"Sisi si madaktari. Na kama Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Bi Hillary Clinton alivyosema jana, sisi tuko hapa na Sanaa na tunafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa tunaleta mabadiliko kwa utaratibu, amani na

Upinzani na vyombo vya sheria Tanzania


Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe ambaye alikamatwa na polisi mjini Dar es Salaam kwa madai ya kuruka dhamana hatimaye alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi iliyopo Arusha kaskazini mwa nchi hiyo siku ya Jumatatu.
Bw Mbowe alitiwa mbaroni na polisi ambao wanadai walikuwa wakitekeleza amri ya mahakama iliyotoa hati ya kumkamata. Hata hivyo kumekuwa na malumbano nchini humo kuhusu utaratibu wanaotumia polisi kuwakamata wabunge wa upinzani.
Hadi sasa wabunge wanane wa upinzani wameshakamatwa kwa makosa mbalimbali.
Kutoka Dar es Salaam mwandishi wetu John Solombi aliandaa taarifa.

Monday, June 6, 2011

Bajeti ijayo haiitambui mikoa mipya, Sunday, 05 June 2011 21:34

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo
Boniface Meena
BAJETI inayotarajiwa kusomwa bungeni Juni 8, mwaka huu inaonyesha kuwa mikoa mipya iliyoanzishwa haijatengewa fedha za kuiendesha kwa mwaka wa fedha ujao.

Mikoa hiyo mipya ni Njombe, Simiyu na Geita ambayo kusudio la kuanzishwa kwake lilitangazwa bungeni mjini Dodoma mwaka jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akihitimisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti kwa ofisi yake.

Kwa mujibu wa mapendekezo yaliyowasilishwa katika Kamati ya Bunge ya Katiba Sheria na Utawala, mikoa iliyotajwa katika Bajeti ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), mikoa iliyotengewa mafungu ni 21 tu.

Kati ya mikoa hiyo, Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na bajeti kubwa ya Sh 213.8 bilioni huku Lindi ukishika mkia kwa kuwa na bajeti ndogo ya Sh 56.0 bilioni.Mbali ya Dar es Salaam mingine iliyotengewa fedha nyingi ni Mwanza (Sh175.6 bilioni), Mbeya (Sh163.4 bilioni), Shinyanga (Sh141.3 bilioni) na Kilimanjaro wenye Sh138.0 bilioni.

Mikoa inayoungana na Lindi kwa kutengewa bajeti ndogo ni Rukwa Sh63.9 bilioni, Singida Sh63.8 bilioni, Mtwara Sh78.2 bilioni na Kigoma Sh72.3 bilioni.

Bajeti kwa mikoa yote hiyo 21 ya Tanzania Bara ni kiasi cha Sh2.3 trilioni.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alipoulizwa kuhusu suala la mikoa hiyo

U-23 yaichapa Nigeria 1-0.

Monday, 06 June 2011 10:46
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana U/23, Thomas Ulimwengu ( kulia) pamoja na Jamary Mnyate kushoto wakijaribu kumdhibiti beki wa Nigeria, Edet Ibok wakati wa mechi ya kimaataifa iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Sweetbert Lukonge
MSHAMBULIAJI  Thomas Ulimwengu aliibuka shujaa baada ya kuifunga bao pekee timu ya taifa ya vijana U-23 Tanzania ilipoichapa Nigeria 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ulimwengu ambaye hivi karibuni alikuwa kwenye majaribio na klabu ya Hamburg ya Ujerumani alifunga bao hilo dakika ya 83, akimalizia vizuri krosi ya Mcha Khamis aliyeingia dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Kigi Makasi.

Pamoja na ushindi huo wa timu ya taifa ya vijana U-23 jana shukrani nyingi kwa kipa Juma Abdul kwa kuonyesha ustadi mkubwa wa kuziba pengo la Shabaan Kado aliyekuwa akidakia Taifa Stars dhidi ya Jamhuri ya Afrika Kati.

Abdul kipa bora wa mashindano ya Kili Taifa Cup alithibisha ubora wake kwa kuokoa hatari kadhaa zilizofanywa na washambuliaji wa Nigeria iliyokuwa imetawala sehemu kubwa ya mchezo huo.

Tanzania iliushangaza ulimwengu pale ilipowatoa washindi wa medali ya dhahabu wa mwaka 2000, Cameroon kwa mikwaju ya penalti kabla ya kuivaa Nigeria washindi wa dhahabu wa mwaka 1996 na fedha 2008.

Mshindi wa mechi ya marudiano watafuzu kwa ligi ndogo hapo mwezi Desemba ili kupata timu tatu zitakazofuzu kwa

Ndege yaanguka ikipeleka wagonjwa Samunge, Sunday, 05 June 2011 21:26, waliofariki samunge wafikia 103, maelfu ya watu kutoka Afrika ya Mashariki, Asia na Ulaya wazidi kumiminika kwa BABU.


Mussa Juma, Arusha
NDEGE ndogo ya abiria, iliyokuwa imebeba wagonjwa kuwapeleka Samunge kwa Mchungaji mstaafu Ambilike Mwasapila, imeanguka na wagonjwa kuwajeruhiwa.
Tukio hilo lilitokea juzi mchana, baada ya ndege hiyo ambayo hufanya safari za Arusha- Loliondo, kupoteza mwelekeo na kuanguka Kijiji cha Mgongo Mageri, Kitongoji cha Melau.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Pwapwa, alithibitisha taarifa za ajali hiyo na kwamba, ndege hiyo namba C150 imesajiliwa kwa namba 54MW0.
Mpwapwa alisema taarifa ambazo zilifika polisi, ndege hiyo ilikuwa na watu wawili ambao ni Emmanuel Swai (74), ambaye amevunjika mkono na rubani wa ndege hiyo, Clinton Swai (25), aliyeumia kichwa.
Alisema wagonjwa hao baada ya ajali hiyo, walikimbizwa Hospitali ya Selian mjini Arusha kupata matibabu.

Waliofariki Samunge wafikia 103
Watu wengine wawili, wamefariki dunia juzi Samunge, huku wakifanya idadi ya

Mbowe huru, polisi watumia ndege ya JWTZ kumsafirisha, Monday, 06 June 2011 21:17

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa amebebwa na wafuasi wa chama hicho, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kukubali dhamana ya kesi yake, muda mfupi baada ya kufikishwa Arusha akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi. Picha na Mussa Juma
Waandishi Wetu, Arusha na   Dar
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe jana aliachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, baada ya kusomewa mashtaka ya kutotii amri halali ya kuhudhuria mahakamani katika kesi inayomkabili ya kufanya mkusanyiko wa watu bila ya kibali na vitendo vya uchochezi.Aidha, mahakama hiyo imemkataa mdhamini wake wa awali, Julius Margwe baada ya kuwa na shaka na mwenendo wake. Diwani wa Kata ya Elerai (Chadema), John Bayo alijitokeza na kuwa mdhamini mpya wa Mbowe.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa alisema mdhamini huyo amekataliwa kutokana na kukiuka masharti ya kuhudhuria mahakamani hapo pamoja na kukabiliwa na kesi katika Mahakama ya Mwanzo Maromboso hivyo, kuamua kutoa nafasi kwa mdhamini mwingine.

 Juzi, Mbowe alisafirishwa chini ya ulinzi hadi Arusha akitokea Dar es Salaam baada ya kukamatwa na polisi. Akizungumzia safari hiyo, Mbowe alidai kuwa alipelekwa kwa ndege ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) usiku wa manane huku akisindikizwa kwa magari manne ya askari wa kutuliza ghasia, kuanzia Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) hadi mahakamani hapo huku akilalamikia hali hiyo na kusema ni matumizi makubwa ya fedha na rasilimali za umma.

"Wamenisafirisha kuja Arusha kwa ndege ya JWTZ kama mtuhumiwa wa ujambazi. Haya ni matumizi makubwa ya