Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akichangia bungeni, makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2011/2012, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
Kizitto Noya, Dodoma
MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa ameiambia Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwa inasumbuliwa na ugonjwa wa woga katika kutoa uamuzi magumu na matokeo yake mambo yake mengi hayaendi kama yalivyopangwa.Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza katika utawala huu wa awamu ya nne, pia akaitaka Serikali hiyo kubadilika.
Alisema kuwa ni bora kulaumiwa kwa kufanya uamuzi mgumu kuliko kulaumiwa kwa kutofanya uamuzi na kwamba Serikali inapaswa kufanya maamuzi bila kujali matokeo yake huku akipendekeza kwa kuanzia, ikope kwa kutumia rasilmali za nchi.
Alitoa kauli hiyo wakati akichangia hotuba ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2011/2012.
"Ni bora kulaumiwa kwa kufanya maamuzi kuliko kulaumiwa kwa kutofanya maamuzi kabisa,"alisema Lowassa.
Bila kueleza ni maamuzi gani ambayo serikali hiyo imeshindwa kufanya, Lowassa alisema ugonjwa wa viongozi kuogopa kufanya maamuzi ni hatari kwa uchumi wa taifa kwa kuwa kuthubutu ni msingi wa mafanikio katika nyanja mbalimbali kijamii na kiuchumi.
"Kuna ugonjwa wa kutokutoa maamuzi hapa na lazima tukubali kubadilike. Ni heri mtu ukosee kutoa maamuzi kuliko kukaa kimya kabisa, heri uhukumiwe kwa kutoa maamuzi kuliko ulaumiwe kwa kushindwa kutoa maamuzi,"alisema.
Lowassa alitoa kauli hiyo huku serikali ikionekana kushindwa kutatua matatizo mbalimbali yaliyoko nchini hivi