| ||
NYOTA wa Manchester United, Wayne Rooney amesema kikosi chake kimetoa somo kubwa kwa majirani zao baada ya kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye mechi ya kuwania Ngao ya Hisani iliyochezwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Wembley. Manchester City walikuwa mbele kwa mabao 2-0 lakini Manchester United walikaza msuli na kufunga mabao matatu. "Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani timu yetu ni bora,''alisema Rooney "Tulitawala mechi nzima, tumewaonyesha kwamba sisi ni zaidi. Sisi ni mabingwa na tulitaka kuthibitisha hilo |
Tuesday, August 9, 2011
Fundisho: Rooney ajipanga kuitesa zaidi Man City.
SIMBA DAY: Simba! Simba! Aaah!
venance.chadema@yahoo.com
SIMBA..Simba! Aaah! Ndiyo kilichotokea wakati mashabiki wa Simba wakishangilia pasi za timu yao ilipocheza na Victors ya Uganda lakini ghafla wakanywea. Kikosi kikicheza kwa mara ya kwanza kikiwa kamili baada ya usajili kukamilika ndani ya ardhi ya Tanzania Bara, Simba ilionyesha mabadiliko lakini ikalala kwa bao 1-0 mbele ya Victors ya Uganda jana Jumatatu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Kocha Moses Basena alilaumu washambuliaji wake kwa kuwataja kwa majina Uhuru Seleman, Emanuel Okwi na Felix Sunzu kwa kukosa nafasi za wazi ambazo zingeweza kuwapa raha zaidi mashabiki katika mchezo huo ambao beki wa zamani wa Simba, Joseph Owino alikuwa jukwaani akishuhudia |
Harusi ya Mercy Johnson yanukia
venance.chadema@yahoo.com
yamembadilikia, imedaiwa kuwa mchumba wake alimficha mambo mengi kuhusiana na mkewe wa zamani na sasa ameyagundua. Alichogundua ni kwamba mumewe alifunga harusi kabisa na mwanamke huyo ingawa alimwambia Mercy kwamba ni feki zilikuwa ni picha za magazetini tu za kutengeneza. Lakini msanii huyo amekasirika na kutishia kwenda kanisani kufuta ndoa hiyo kama hataweka mambo wazi na kusema kila kitu kilichojiri, lakini inadaiwa ndugu wa mumewe wanahangaika kuweka mambo sawa. |
Rooney: Tumewaonyesha City sisi ni mabosi
venance.chadema@yahoo.com
| Monday, 08 August 2011 20:44 |
MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney amesema timu yake imewaonyesha wapinzani wao Manchester City kwamba nani ni bosi nchini England baada ya juzi kuwachapa mabao 3-2 na kutwaa Ngao ya Jamii. "Matokeo haya yanaonyesha ni timu ipi bora, katika mechi nzima tulitawala sisi na hata tofauti iliyoonyeshwa na wachezaji wetu vijana ilikuwa kubwa, tuliwasambaratisha, matokeo tuliyopata tunastahili, sisi ni mabingwa, tulitakiwa kushinda na tulitakiwa kuthibitisha hilo,"alisema |
Warembo Miss Tanzania waingia kambini
| |
| Monday, 08 August 2011 20:47 |
| Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza alisema kuwa sababu kubwa ya kuanzisha utaratibu mpya ni kuwapa nafasi zaidi warembo hao kujifunza mambo mengi wakiwa kambini kama mashindano ya “Big Brother Africa”. Rwehumbiza alisema kuwa mfumo huu ni tofauti na ule uliozoeleka |
Viongozi CUF wanusurika ajalini
venance.chadema@yahoo.com
| |
| Monday, 08 August 2011 21:27 |
| Ajali hiyo ilitokea jana jioni kilomita karibu 10 kutoka mjini Morogoro barabara ya kuelekea Dar es Salaam na kumsababishia majeraha kiongozi huyo na abiria wake. Akizungumza na Mwananchi jana jioni katika eneo la ajali Mtatiro alisema kuwa gari waliyokuwa nayo aina |
venance.chadema@yahoo.com
| Mtoto aliyeibwa Bunda miaka saba iliyopita apatikana nchini Kenya |
| Sunday, 07 August 2011 21:50 |
| Mtoto huyo wa kiume Nyambibiti Lazaro, ambaye sasa hajui lugha yoyote tofauti na kijaluo, aliibwa na mwanamke wakati huo akiwa na umri wa miezi minne, wakati mama yake mzazi alipokuwa amemwacha nyumbani kwao, akiwa chini ya uangalizi wa mtoto mwenzake mwenye umri wa |
Madiwani waliotimuliwa Chadema wajipanga kwenda mahakamani .
venance.chadema@yahoo.com
| |
| Monday, 08 August 2011 21:28 |
| Uwezekano huo ulielezwa na Diwani wa Kata ya Elerai, John Bayo, alipozungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kutokea Dodoma walipokwenda kuhojiwa kabla ya uamuzi wa kutimuliwa kufikiwa. “Binafsi sina kinyongo na chama changu wala viongozi wake. Nimepokea uamuzi huo kwani ndiyo msimamo wa vikao, lakini nakuhakikishia bado nina imani ya kuendelea na nafasi yangu ya udiwani hadi uchaguzi mkuu ujao, kuna njia nyingine ya kupinga uamuzi huo kupitia vikao au |
Uchunguzi tuhuma za Jairo ngoma nzito
venance.chadema@yahoo.com
| Monday, 08 August 2011 21:30 |
| MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amesema uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, unaendelea na siku kumi zilizotolewa hazitoshi. Awali, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, akizungumzia hatua za haraka za Serikali kushughulikia kashfa hiyo, ilisema uchunguzi huo dhidi ya Jairo ungetumia siku 10, lakini Julai 31, ambayo ilikuwa ni siku ya kumi, CAG Utouh alisema ndiyo kwanza alikuwa na siku ya tano tangu kuanza ukaguzi. Akizungumza Dar es Salaam jana, Utouh alisema uchunguzi siyo kuandika ripoti, kwani |
Serikali, wauza mafuta sasa wafikia pabaya .
venance.chadema@yahoo.com Monday, 08 August 2011 21:35
[Kituo cha kuuzia mafuta cha BP Upanga kikiwa tupu kutokana na kile kianchoelezwa kuIshiwa na mafuta, kwa zaidi ya siku nne vituo vinavyomilikiwa na BP haviuzi mafuta, bada ya mgomo uliondeshwa nchi nzima na wauza mafuta waking EWURA kupunguza bei ya bidhaa hiyo kutokana na serikali kuwapunguzia kodi ilikuleta unafuua kwa wananchi. Picha na Fidelis Felix ] Kituo cha kuuzia mafuta cha BP Upanga kikiwa tupu kutokana na kile kianchoelezwa kuIshiwa na mafuta, kwa zaidi ya siku nne vituo
[Kituo cha kuuzia mafuta cha BP Upanga kikiwa tupu kutokana na kile kianchoelezwa kuIshiwa na mafuta, kwa zaidi ya siku nne vituo vinavyomilikiwa na BP haviuzi mafuta, bada ya mgomo uliondeshwa nchi nzima na wauza mafuta waking EWURA kupunguza bei ya bidhaa hiyo kutokana na serikali kuwapunguzia kodi ilikuleta unafuua kwa wananchi. Picha na Fidelis Felix ] Kituo cha kuuzia mafuta cha BP Upanga kikiwa tupu kutokana na kile kianchoelezwa kuIshiwa na mafuta, kwa zaidi ya siku nne vituo
Spika amtwisha Zitto Kabwe zigo la UDA.
venance.chadema@yahoo.com
| Monday, 08 August 2011 23:06 |
| SAKATA la kuuzwa kwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) limezidi kugonganisha vichwa vya mamlaka mbalimbali, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhamisha mchakato wa uchunguzi huo kutoka Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwenda Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).Utata wa uuzaji wa shirika hilo umesababisha pia mvutano mkubwa kati ya wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam na Meya wa jiji hilo, Dk Didas Masaburi ambaye wiki iliyopita aliwashambulia wawakilishi hao kwa maneno makali huku akitoa vitisho kwamba atalipua tuhuma zao za ufisadi. Makinda aliikabidhi jukumu hilo POAC Ijumaa ya Agosti 5, Spika na kuliondoa Kamati ya Miundombinu ambako Profesa Juma Kapuya ambaye ni mmoja wa wajumbem, ana maslahi na UDA kutokana na kuwa mmoja wa wanahisa wa Kampuni ya Simon Group. Kaimu Katibu wa Bunge John Joel alithibitisha jana Spika amefanya |
Monday, July 18, 2011
Chadema wamuundia tume John Shibuda .
venance.chadema@yahoo.com
| Monday, 18 July 2011 21:34 |
| CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeunda tume itakayoongozwa na Profesa Abdallah Safari kumhoji Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu zinazomkabili. Hii ni mara ya pili kwa Shibuda kuhojiwa na jopo maalumu la Chadema kwani tayari aliwahi kuhojiwa baada ya kupingana na msimamo wa chama hicho wa kumsusia Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizundua Bunge Desemba mwaka jana kwa kuhudhuria dhifa katika Ikulu ya Chamwino huku akiweka bayana kupingana na msimamo huo. Mapema mwezi huu alitoa tena kauli ambazo Chadema imeziita ni |
Shellukindo ailipua Wizara ya Ngeleja .
venance.chadema@yahoo.com
| |
| Monday, 18 July 2011 21:36 |
| MBUNGE wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo amelipua bomu Bungeni akimtuhumu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, kwa kutumia zaidi ya Sh 1 bilioni kwa ajili ya kutoa rushwa kwa watu mbalimbali ili bajeti ya wizara hiyo iweze kupitishwa na Bunge.Tuhuma hizo nzito zinakuja kipindi ambacho tayari Wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini wakiwa wameibua tuhuma kama hizo za baadhi ya wajumbe kutaka kuhongwa na maofisa wa wizara hiyo, ili kurahisisha upitishaji wa bajeti ndani ya kamati. Takriban wiki tatu tangu wabunge wa kamati hiyo kuibua tuhuma |
Friday, July 15, 2011
LAPF yaongeza uwekezaji hadi sh. bilioni 265.9
venance.chadema@yahoo.com
MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF) umeongeza uwekezaji kutoka sh. bilioni 154.5 kuanzia Juni 2008 hadi kufikia sh.bilioni 265.9 ilipofika
Juni mwaka huu.
Akizungumza katika Mkutano na Ujumbe Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)na balozi mdogo wa Kenya nchini Kenya, aliyetaka kujua muundo wa mfuko huo, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji LAPF, Bi, Rose Metta, alisema uwekezaji umezidi kukua kwa asilimia 106.
Akieleza upatikanaji wa fedha hizo,
Bi. Metta alisema zinatoka kwenye michango ya wanachama, mapato
Juni mwaka huu.
Akizungumza katika Mkutano na Ujumbe Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)na balozi mdogo wa Kenya nchini Kenya, aliyetaka kujua muundo wa mfuko huo, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji LAPF, Bi, Rose Metta, alisema uwekezaji umezidi kukua kwa asilimia 106.
Akieleza upatikanaji wa fedha hizo,
Bi. Metta alisema zinatoka kwenye michango ya wanachama, mapato
Uhuru:Tujenge timu, hakuna aliyehongwa.
| Thursday, 14 July 2011 22:19 |
| WINGA wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba, Uhuru Selemani amewasihi mashabiki na viongozi wa timu hiyo kuacha tabia ya kuwahukumu wachezaji kwamba walihujumu na kufungwa na wapinzani wao Yanga bao 1-0 kwenye fainali ya Kombe la Kagame iliyofanyika Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kauli ya nyota huyo ambaye hivi karibuni amerejea dimbani baada ya kupona goti lililokuwa linamsumbua inafuatia kitendo cha baadhi ya mashabiki wa Simba kuwatuhumu baadhi ya wachezaji kuwa ndio sababu ya timu yao kufungwa na Yanga siku ya fainali. Wachezaji wa Simba wanaoshutumiwa na mashabiki kuwa walifanya hujuma na kuchangia timu hiyo kufanya vibaya ni kiungo Mohamed Banka, mshambuliaji Musa Hassan Mgosi na beki Kelvin Yondani. Simba ilikuwa haipewi hata nafasi ya kufika kwenye raundi ya pili kutokana na kuwa na kikosi dhaifu baada ya kutimua nyota wake wengi siku chake kabla ya michuano hiyo, lakini wachezaji hao waliweza kupigana na kufika fainali. Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana Uhuru alisema |
Tanesco waingiza mitambo ya kufulia umeme.
| Thursday, 14 July 2011 22:12 |
| SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limeanza kuingiza mitambo yenye thamani ya Dola 120 milioni za Marekani kwa ajili ya kufulia umeme, katika Mkoa wa Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Meneja Mahusiano kwa Umma katika Tanesco, Badra Masoud, mitambo hiyo itatumia gesi asilia kuzalishia umeme kwa kiwango cha megawati 100. Alisema kwa sasa shirika lina upungufu wa megawati 250 za umeme yakiwa ni matokeo ya kupungua kwa kina cha maji katika Mabwawa ya Kidatu na Mtera. Badra ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alisema tayari shirika limeshaingiza mtambo mmoja na mingine miwili itaingia wakati wowote kuanzia sasa. Pia alisema kiwango cha mgawo wa umeme kimeongezeka kwa saa 18 badala ya 12 na kwamba hiyo inatokana na sababu za kitaalamu, zilizolilazimisha shirika kuzima mitambo ya uzalishaji. "Wananchi wamekosa imani na Tanesco hata wanapotuona hii ni kutokana na |
Washtakiwa 31 ‘samaki wa Magufuli’ waachiwa.
| Send to a friend |
| Thursday, 14 July 2011 22:25 |
| JUMLA ya washtakiwa 31 kati ya 36 waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania maarufu kama kesi ya samaki wa Magufuli wameachiwa huru. Washtakiwa hao kutoka Mataifa ya China, Ufilipino, Vietnam na Kenya walikuwa wakituhumiwa kufanya shughuli za uvuvi katika eneo hilo bila kuwa na kibali na kuchafua mazingira ya bahari katika eneo hilo. Lakini jana Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaa mbele ya Jaji Augustine Mwarija anayesikiliza kesi hiyo iliwaachia huru washtakiwa hao baada ya kuridhika kuwa hawana kesi ya kujibu kuhusiana na tuhuma zilizokuwa zikiwakabili. Wakati wakiachiwa huru jana washtakiwa hao walikuwa wameshasota mahabusu kwa muda wa miaka miwili na miezi minne tangu walipokamatwa Machi 9 hadi walipoachiwa huru jana.Wakati 31 wakiachiwa huru kwa kutokuwa na kesi ya kujibu washtakaiwa wengine watano wamepatikana na kesi ya kujibu na hivyo mahakama kuwataka wajitetee kuhusiana na tuhuma hizo. Waliopatikana na kesi ya kujibu ni pamoja na mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo Hsu Chin Tai ambaye ni Nahodha wa meli waliyokuwa wakiitumia kwa shughuli za uvuvi. Wengine ni mshtakiwa wa saba Zhao Hanquing, mshtakiwa wa tisa Hsu Sheng Pao ambao wote ni mawakala wa meli hiyo, pamoja na wahandisi wawili wa meli hiyo Cai Dong Li mshtakiwa wa 33 na Chen Rui Hai mshtakiwa wa 34. Akisoma uamuzi wake jana Jaji Mwarija alisema kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka hususani ushahidi wa shahidi wa tatu Nahodha Ernest Bupamba kutoka Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi ameridhika kuwa washtakiwa hao wana kesi ya kujibu. Bupamba ambaye ni Ofisa msimamizi wa sheria na shughuli za uvuvi katika ushahidi wake aliieleza mahakama kuwa ndiye aliyewakamata wakati wakifanya doria na timu ya wanadoria kutoka mataifa matatu. Mbali na ushahidi wake wa mdomo kuwa rada aliposoma kwenye rada iliyokuwa kwenye meli yao ya doria ilionyesha kuwa walikuwa katika eneo la Tanzania, pia Nahodha Bupamba aliwasilisha mahakamani vielelezo huku akiwasilisha mahakamani vilelezo vya picha zinazohusiana na mashtaka hayo. Tai (nahodha), Li na Hai (wahandisi) wakipatikana na kesi ya kujibu katika kosa la kwanza la kufanya shughuli za uvuvi katika Ukanda wa Bahari Kuu ya Tanzania bila kuwa leseni na kosa la pili la kuchafua mazingira ya bahari kwa uchafu wa samaki na mafuta ya meli. Kwa upande wao Hanquine na Pao (mawakala) wao walipatikana na kesi ya kujibu katika kosa la tatu ambalo ni kosa mbadala wa kosa la kwanza na la pili, yaani kosa la kutaka kuwasaidia washtakiwa wengine wakwepe mashtaka(Accessory after the fact). Katika shtaka hilo la tatu washtakiwa hao wanatuhumiwa kuwa baada ya washtakiwa wengine kukamatwa washtakiwa hao walifika nchini wakiwa na leseni na hati za meli ili kuonyesha kuwa walikuwa wakifanya shughuli za uvuvi kihali ili wapone katika mashtaka hayo. Kabla ya kuwaachia hao 31 na kuwakuta na kesi ya kujibu watano kwanza Jaji Mwarija alianza kwa kurejea majumuisho ya hoja za pande zote na kuanza kuchambua moja baada ya nyingine, huku akitupilia mbali na kukubaliana na baadhi ya hoja za pande hizo zote. Baada ya kufanya uchambuzi wa hoja hizo Jaji Mwarija alisema kuwa ameridhika kuwa kwa jinsi inavyoonekana kutokana na ushahidi uliopo upande wa mashtaka umethibitisha kesi katika shtaka la kwanza na pili. “Lakini swali la kujiuliza ni kwamba ni kwa nani upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha kesi katika makosa hayo,” alijihoji Jaji Mwarija.Alisema hakubaliani na upande wa mashtaka kuwa umethibitisha kesi katika mashtaka hayo kwa kila mshtakiwa. Aliongeza kuwa ushahidi wa washtakwa wote kukutwa tu ndani ya meli hautoshi kwani majukumu ya kila mmoja katika meli hayakuwekwa wazi na kwamba upande wa mashtaka ulipaswa kuliweka wazi, kwani si kweli kwamba wote walikuwa wakivua samaki. “Kigezo katika shtaka la kwanza ni kuvua bila kuwa na leseni. Lakini kuna ushahidi kwamba wengine walikuwa ni wapishi ndani ya meli ile,” alisema Jaji Mwarija na kuongeza kuwa kwa mujibu wa shahidi wa sita (PW6) suala la leseni ni jukumu la nahodha. |
Mchumba wa Slaa avamiwa, aporwa.
| Thursday, 14 July 2011 22:27 |
| JOSEPHINE Mushumbushi, ambaye ni mchumba wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa, amevamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kuporwa simu mbili, kamera na fedha taslimu sh 50,000. Tukio hilo ambalo lilitokea jijini Dares Salaam juzi, karibu na SUMA-JK, ni mwendelezo wa wimbi la matukio ya uhalifu wa kutumia pikipiki maarufu kama bodaboda. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alifafanua kwamba tukio hilo lilitokea juzi mnamo saa 11:57 jioni, wakati Mushumbushi akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Harrier lenye |
Lowassa: Nimeshtushwa.
| Send to a friend |
| Thursday, 14 July 2011 22:42 |
| WAKATI uamuzi wa Rostam Aziz kung'atuka ubunge wa Igunga na ujumbe wa Halmashauri Kuu (Nec) ndani ya chama chake cha CCM ukiibua gumzo kubwa karibu kila kona nchini, mshirika wake mkubwa kisiasa, Edward Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli ameeleza kushtushwa na tukio hilo.Juzi, Rostam, mmoja wa watu muhimu ndani ya CCM aliyeshiriki vyema katika mtandao uliomwingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete mwaka 2005, alitangaza uamuzi mzito wa kung'atuka siasa akipinga kile alichokiita siasa uchwara za baadhi ya viongozi wake.Uamuzi huo mzito wa Rostam uliibua kwikwi na vilio kutoka kwa wapigakura jimboni kwake Igunga, wakiwamo wale waliomchagua kwa vipindi vitatu mfululizo tangu mwaka 1994 ulipofanyika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Charles Kabeho. Jana, Lowassa alisema: "Kwa kweli nimeshtushwa, nimesikitishwa...kilichonishtua zaidi ni vilio. Namna wananchi wa Igunga walivyokuwa wanalia na kusikitika." Hata hivyo, Lowassa ambaye naye amekuwa akitajwa katika orodha ya |
Subscribe to:
Posts (Atom)


