Mlinda lango kutoka Marekani, Brad Friedel, amekubali kujiunga na klabu ya Tottenham.
Kipa wa Villa kuichezea Tottenham
Sasa inafahamika kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40, ambaye mkataba wake na klabu ya soka ya Aston Villa ulitazamiwa kwisha mwishoni mwa mwezi huu, ametia saini mkataba wa miaka miwili na Tottenham.
Meneja wa Tottenham, Harry Redknapp amesema: "Ni vyema kuwa na walinda lango wazoefu watatu katika klabu [Heurelho] Gomes, Carlo [Cudicini] na sasa Brad.
"Inamaanisha kutakuwa na ushindani katika kuwania nafasi kucheza, hasa kutokana na mechi nyingi tunazozitazamia msimu ujao".
Friedel, ambaye atapatikana pasipo ada yoyote, ana uzoefu mkubwa katika